Nenda kwa yaliyomo

Hafiz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 07:12, 8 Julai 2019 na Riccardo Riccioni (majadiliano | michango)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)

Makala hii inasema juu ya watu wanaoshika Qurani yote moyoni; kwa watu walioitwa Hafez / Hafiz n.k. angalia hafiz (maana)

Hafiz (kutoka Kiarabu حافظ ḥāfiẓ -kitenzi حفظ ḥāfaẓa = "kuhifadhi, kutunza") ni cheo cha heshima katika Uislamu kwa kumtaja mtu aliyeishika Qurani yote moyoni. Mwanamke au binti aliyeishika msahafu huitwa "hafiza".

Hafiz anajua kusema maneno yote ya Qurani. Mtu wa aina hii huheshimiwa sana kati ya Waislamu. Mara nyingi ni watu vipofu au walemavu wanaoanza kushika maneno ya Qurani tangu utoto maana kwao ni njia mmoja ya kuheshimiwa pia kuwa na mapato kwa sananu mahafiz hualikwa mara nyingi kuimba surat za Qurani wakati wa sherehe na siku maalumu.

Mahafiz wa kwanza wanasemekena walitokea katika siku za kwanza za Uislamu kwa sababu mwanzoni Qurani ilitangazwa na mume Muhammad kama hotuba tu hapakuwa na utaratibu wa kuiandika. Lakini watu wengi walishika maneno haya. Baadaye Khalifa Umar aliagiza Qurani yote kuandikwa na katika kazi hii mahafiz walikuwa muhimu walioweza kurudia surat kwa waandishi.

Hata baada ya Qurani iliandikwa bado mahafiz walitafutwa kwa sababu Waislamu wengi hawakujua kusoma tena kwa sababu namna yao ya kuimba maneno ya surat uliwavuta watu. Kati ya watoto wanaoanza kujifunza Qurani katika madrasa wanjitokeza mara kwa mara kadhaa wanaoelekea kuwa hafiz.

Kutokana na heshima ya cheo hiki kimetumiwa mara nyingi kama jina kati ya Waislamu ikiandikwa pia Hafez, Hafes, au Hafis kutegemeana na lugha ya mazingira.