Kamchatka
Mandhari
Rasi ya Kamchatka (rus. полуо́стров Камча́тка poluostrov Kamchatka) ni rasi kwenye upande wa wa mashariki ya Urusi. Ina urefu wa kilomita 1,250 na eneo la 270,000 km².[1]
Imeenea katika Bahari Pasifiki ikitenganisha Bahari ya Okhotsk na Pasifiki kubwa.[2]
Volkeno za Kamchatka zimeandikishwa katika orodha ya UNESCO ya urithi wa dunia.
Kiutawala ni sehemu ya mkoa wa Kamchatka Krai mwenye wakazi 322,079. Zaidi ya nusu ya wakazi hawa wanaishi katika miji miwili ya Petropavlovsk-Kamchatsky (waakzi 179,526) na Yelizovo (38,980).
Marejeo
- ↑ Быкасов В. Е. Ошибка в географии // Известия Всесоюзного Географического Общества. — 1991. — № 6. (Kirusi)
- ↑ "Kamchatka Peninsula". Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 2008-02-20.
- Gleadhill, Diana (2007), Kamchatka: A Journal & Guide to Russia's Land of Ice and Fire, Hong Kong: Odyssey Books, ISBN 978-962-217-780-2.
Viungo vya Nje
Wikimedia Commons ina media kuhusu: