Angelina Jolie
Angelina Jolie | |
---|---|
| |
Jina la kuzaliwa | Angelina Jolie Voight |
Alizaliwa | 4 Juni 1975 Marekani |
Kazi yake | Mwigizaji Mtayarishaji Mwongozaji |
Miaka ya kazi | 1982 - |
Ndoa | Jonny Lee Miller (1996-1999) Billy Bob Thornton (2000-2003) Brad Pitt (2014-2019) |
Watoto | 6 |
Wazazi | Jon Voight, Marcheline Bertrand |
Angelina Jolie (alizaliwa tar. 4 Juni 1975) ni mwanamitindo wa zamani, mwigizaji wa filamu na pia mfadhili, wakala wa wakimbizi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa (UN). Ni mwanamama anayetajwa mara kwa mara kwenye vyombo habari kwamba ni mzuri zaidi.
Maisha ya awali na familia
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa kwa jina Angelina Jolie Voight huko mjini Los Angeles, California, Marekani, akiwa kama binti wa waigizaji John Voight na Marcheline Bertrand, ambaye alifariki 27 Januari 2007 kwa ugonjwa wa saratani.
Jolie pia ni mpwa wa mshairi, mwanamuziki "Chip Taylor" maarufu kama James Wesley Voight, na pia ni dada wa mwigizaji wa filamu James Haven. Asilia ya Jolie kwa upanda wa baba ni Mslovak na Mjerumani asilia, na kwa upande wa mama yake ni Mfaransa na Mkanada wenye jamii ya Iroquois", japokuwa mama yake Jolie aliwahi kudai uataifa wa kuwa Mmarekani uliamuliwa na mumewe Voight.
Ilivyofika mwaka 1976 mwaka mmoja toka anglelina azaliwe baba na mama yaek jolie wakatengana hivyo joilie na kaka yake wote walikulia kwa malezi ya mama, na kuwatelekeza kwenye mradi wa Ugizaji kisha kuhamia nao wote Mjini Palisades, New York.
Alivyokuwa mtoto Jolie alikuwa anakawaida ya kuangalia filamu mara kwa mara na mama yake na baadae kuelezea kwamba hii inaashilia kwamba mapenzi ya Jolie ni kuwa Muigizaji, japokuwa hakuvutiwa na uigizaji wa baba yake.
Alivyofikia umri wa miaka 11 Familia ilirudi tena Los Angeles na Jolie akamua kuwa anataka kuigiza na akaenda kujiandikisha katika taasisi ya uigizaji ya 'Lee Strasberg' maarufu kama "Strasberg Theatre Institute", Ambako alipata mafunzo kwa muda wa miaka miwili na baadae kuonekana kwenye maigizo ya jukwaa kadha wa kadha.
Baada hapo Jolie akamua kutumia muwa wake kama mwanafunzi katika shule ya "Beverly Hills High School"(Jina Jipya Moreno High School), akiwa shule jolie fikra zake zilikuwa ni kukaa mbali na watoto wa famlia za matajiri.
Mama yake Jolie alikuwa akiridhika na kipato chake alichokuwa anapata japokuwa kilikuwa cha hali ya chini na Jolie alikuwa akivaa nguo za mitumba. Alikuwa akilizwa sana na baadhi ya wanafunzi wenzake waliokuwa wakimuonyeshea kidole na kumcheka kwa kuwa alikuwa mwembamba sana na mtindo wake wa kuvaa miwani na gango. Heshima yake ilipungua sana pale alijaribu kutaka kuanza masuala ya Uanamitindo na kutoka bila mafanikio.
Na pia Jolie alikuwa tofauti kabisa na baba yake hasa kwa kitendo cha kutokuwa mwaminifu na kuvunja familia yake, japokuwa kipindi fulani walijaribu kupatanishwa na kuweza kuelewana na baadae kuigiza pamoja katika filamu ya "Lara Croft: Tomb Raider".
Ilivyofika Julai 2002 Jolie alifungua jalada halali la kuomba kubadili jina la "Angelina Jolie" na kulibwaga jina la babake mzee voight kuwa ndio jina la mzee wake, jina la Angelina Jolie lilibadilishwa rasmi 12 Septemba 2002. Mwezi wa Agosti mwaka huo huo baba yake Jolie alikuwa akitangaza kwamba binti yake ana mtindio wa akili katika kituo cha TV cha mjini hollywood maarufu kama "Access Hollywood".
Mwezi Oktoba 2004 toleo la gazeti moja hivi liitwalo Premiere Magazine, liliandika habari kwamba Jolie hana mda tena wala kutaka msaada wowote ule kutoka kwa baba yake mzazi mzee John Voight na kusema kwamba ni baba yake sawa lakini wala hana haja ya kuzungumza nae.
Sina kinyongo nae ila sina imani kama kuna mtu yoyote ambaye yeye ni damu yake (Voight).
kwasabu watoto zake wamelelewa na wamekuwa, sema jolie hakutaka kusema mengi mbele ya hadhara kwasababu ya malumbano na baba yake, kwakuwa mwanawe alimlea mwenyewe bila ya ushirikiano wowote ule na mzee voight basi ana amini kila kitu anaweza kufanya bila ya voight.
Jolie ni ni mwanama jasili na aliyekulia kwenye maisha ya tabu sana wakati baba yake mzazi ana uwezo sema hana mda kuitazama familia, ndio sababu iliyoplekea Jolie kutompenda baba yake.
Mahusiano
[hariri | hariri chanzo]Tarehe 28 Machi Jolie aliolewa na muigizaji filamu wa kiingereza maaurufu kama Jonny Lee Miller, mshirika mwenzie katika filamu ya "Hackers". Aliuzuria harusi yake akiwa amevaa suruali nyeusi ya ngozi na shati leupe, lilochorwa jina la bwana harusi mgongoni kwake.
Baada ya mwaka mmoja Jolie na Miller wakatengana, arafu taraka ilifuata baadae 3 Februari 1999. Wakawa wamebaki kwenye hali nzuri na baadae Jolie alikubali kuwa jamaa alikuwa mume mzuri na msichana anaweza akamtaka 'na nitaendelea kumpenda' kwasababu wote tulikuwa tungali vijana.
Baadae akaolewa tena na muigizaji filamu wa kimarekani "Billy Bob Thornton", ambaye alikutana nae katika filamu ya "Pushing Tin" iliyochezwa mwaka 1999. ilifika tarehe 5 mei 2000, ilikuwa siku ya kutangaza penzi mbele ya hadhara na kufanya mshangao mwingine tena wa kuzungushia baadhi ya vitu kwenye shingo zao, mahusiano yao yakaja kuwa ni mada inayopendwa kuzungumziwa kila mara kwenye vyombo vya habari.
Jolie na Miller waliachana tarehe 27 Mei. Mwanzoi mwa mwaka 2005 Jolie alikubwa na kashfa na kushtakiwa kwamba yeye anahusika na utarikiano baina ya muigizaji Brad Pitt na Jennifer Aniston kuwa Jolie alikuwa mwanamke wa nje wa Brad Pitt hivyo kufunguliwa mashtaka ya kuaribu ndoa yake.
Mahusiano ya Jolie na Pitt yalianza pale walipoigiza filamu pamoja katika filamu ya "Mr. & Mrs. Smith", japokuwa alikuwa akikana mara mara kwa mara kwenye vyombo vya habari aikihojiwa juu ya hilo.
Kwenye mahojiano 2005 na Ann Curry, alieza kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mume wa mtu, wakati baba yake mzazi alimdanganya mamake na mwanamke mwingine kitu ambacho hatoweza kumsamehe. Akasema hakujiangalia mwenyewe asubuhi kama amefanya hicho kitendo cha kutembea na mume wa mtu na wala hakuvutiwa na mwanaume mwenye kumsaliti mkewe.
Wakati Jolie na Pitt hawakuweka bayana asili ya mahusiano yao, ubazazi uliendela na kuishia 2005. Mwandishi wa habari wa siri alipiga picha mwezi Aprili, Mwezi mmoja toka Aneston afungue jalada la utarikiano, nakumuonyesha mwana mama huyo picha ya Jolie na mwanae wa kiume wakiwa kwenye fukwe za nchini kenya akiwa pamoja na Pitt.
Kipindi cha kiangazi Jolie na Pitt walikuwa wakikutana pamoja na kuongezana mara mara kitendo kilipelekaa vyombo vingi vya habari kusema wale mke na mume huku wakijiita "Brangelina".
Mnamo tarehe 11 Januari 2006 Jolie alithibitisha kuwa ana ujauzito wa Brad Pitt na wana mpango wa kuweka bayana uhusiano wao.
Watoto
[hariri | hariri chanzo]Mnamo tarehe 10 Machi,2002, Jolie amemlea mtoto wake wa kwanza Maddox Chivan Jolie-Pitt, (Jina Halisi Maddox Chivan Thornton Jolie).Alizaliwa 5 Augosti 2001, mjini Rath Vibol nchini Kambodia na akanza kuishi katika kituo binafsi cha kulelea watoto yatima cha mjini Battambang.
Jolie akmua kuomba ulezi baada ya kutembela Kamboadia mara mbili wakati akicheza filamu ya "Tomb Raider" na safari ya majaribio ya UNHCR mwaka 2001.
Tarehe 6 Julai 2006, Jolie ameanza kumlea mtoto yatima wa miezi sita kutoka Ethiopia, jina lake Zahara Marley Jolie-Pitt (Jina Halisi Zahara Marley Jolie), ambae wazazi wake walifariki na Ukimwi. Zahara alizaliwa 8 Januari, 2005 kama Tena Adam. Jolie akamchukua mtoto na kumpeleka kwenye ktuo cha kulea watoto yatima kilichopo Addis Ababa.
baadae kidogo akarudi Marekani kwa muda, kipindi chote ambacho Jolie hayupo Ethiopia Zahara alikuwa akiishi Hospitali kwasababu zahara alikuwa na upungufu wa maji mwilini na utapiamlo.
Brad Pitt na Jolie ilitaarifiwa kuwa wametiya saini hati za kulelea mtoto na kisha kumchukua kama mtoto wao rasmi, baadae Pitt akakubali kumlea pamoja mtoto Zahara. Ilivyofika Desemba 2005 ilithibitishwa kuwa Pitt aliomba malezi ya watoto wa waili wa Jolie kiharali, na ilvyofika tarehe 19 Januari 2006 Hakimu wa California alithibitisha ombi hilo. Watoto hao baadae majina ya wazee yakabadilishwa kuwa Jolie-pitt.
27 Mei 2006, Jolie Amejifungua mtoto wa kike aitwaye Shiloh Nouvel Jolie-Pitt aliyezaliwa mjini Swakopmund, Namibia, ni tafsiri kutoka kwenye Biblia, inakuja maana ya "Enye Amani".
Mnamo Tar. 15 Machi 2007, Jolie amemchukua mtoto mwingine wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu, kutoka nchini Vietnam, wakamwita Pax Thien Jolie-Pitt, aliyezaliwa tarehe 29 Novemba 2003 na kutelekezwa katika hospitali za kienyeji, Ambako alipewa jina Pham Quang Sang. Jolie alimchukua mtoto huyo kutoka kwenye kituo cha kulelea watoto yatima kiitwacho Tam Binh orphanage, cha mjini "Ho Chi Minh City". Jina lake jipya ni mchanganyiko wa neno la kilatini "Amani" na la kivietnam "Mawingu" au Mbinguni".
Filamu Alizoigiza
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]
- Jolie Tovuti ya Mashabiki(sio rasmi Ilihifadhiwa 25 Septemba 2020 kwenye Wayback Machine.