Karne ya 19
Lango la Historia | Lango la Biografia | Karibuni | Orodha ya Miaka
◄ |
Karne ya 17 |
Karne ya 18 |
Karne ya 19
| Karne ya 20
| Karne ya 21
Miaka ya 1800 |
Miaka ya 1810 |
Miaka ya 1820 |
Miaka ya 1830 |
Miaka ya 1840 |
Miaka ya 1850 |
Miaka ya 1860 |
Miaka ya 1870 |
Miaka ya 1880 |
Miaka ya 1890
Karne ya 19 ilikuwa kipindi cha miaka mia moja kati ya 1800 na 1900. Kikamilifu kilianza tarehe 1 Januari 1801 na kuishia 31 Desemba 1900.
Kama kila "karne" ni kipindi kinachohesabiwa kwa hiari ya binadamu kwa sababu ni mgawanyo wa kalenda tu - hali halisi, maendeleo na mabadiliko makubwa hayafuati migawanyo ya kalenda ya kibinadamu.
Hata hivyo kipindi hiki cha karne ya 19 kilikuwa kipindi muhimu sana katika historia ya binadamu.
Watu na matukio
[hariri | hariri chanzo]Mabadiliko mengi yalianzia Ulaya na kuenea duniani, hivyo karne hii imeitwa na wataalamu "karne ya Ulaya".
Baadhi ya tabia za pekee za karne hii ni kama zifuatazo:
- Mapinduzi ya viwandani: yaliwahi kuota mizizi katika Uingereza kabla ya 1800, lakini katika karne hii yalienea katika nchi za Ulaya na kuzitofautisha kwa uwezo wao
- Nchi zilizopita katika mapinduzi ya viwandani ziliongezewa nguvu za kiuchumi na za kijeshi kushinda mataifa nje ya mapinduzi haya
- Mtindo wa ubepari ulipata umuhimu na kugusa maisha ya watu wengi
- Tabaka jipya la wafanyakazi lilijitokeza
- Tabaka la makabaila lilipungukiwa umuhimu wake katika jamii za nchi zilizoshiriki katika mapinduzi ya viwandani
- Maisha ya viwandani na maisha ya mjini yalivunja nguvu ya maisha ya mashambani hivyo mapokeo na desturi nyingi zilizoendelea tangu karne nyingi
- matunda ya falsafa ya mwangaza yalisababisha
- kutokea kwa sayansi ya kisasa
- ukosoaji wa dini
- Idadi ya watu duniani ilianza kukua haraka kushinda miaka yote ya historia ya awali kwa sababu ya
- matokeo ya teknolojia na sayansi yaliongeza kiasi cha chakula kilichopatikana kwa watu
- sayansi ya tiba iligundua njia za kupambana na ugonjwa
- Nchi kadhaa za Ulaya zilitumia nguvu mpya ya kueneza utawala wao nje ya Ulaya
- Ukoloni ulienea : mwanzoni mwa karne hii polepole, mwishoni kwa mbio
- Fundisho jipya la "utaifa" lilianza kubomoa misingi ya madola makubwa ya kimataifa katika Ulaya kama Uturuki, Austria, Urusi.
- Katika siasa madola kadhaa yaliyowahi kuratibu maisha ya watu tangu karne nyingi yalipungukiwa, kuvunjwa au kupotea kabisa kama vile:
- Dola Takatifu la Kiroma (Ujerumani) katika Ulaya ya Kati
- Dola la Moghul katika Bara Hindi
- Dola la Uturuki (Uturuki, Afrika ya Kaskazini, Asia ya Magharibi)
- Dola la Hispania (Hispania, Amerika ya Kusini na Ufilipino)
- Dola la Uingereza lilitokea kuwa dola kubwa duniani
- Utumwa ulipungua sana duniani
- Ukristo ulienea upya nje ya Ulaya kwa njia ya misheni za kisasa baada ya kurudishwa nyuma na Uislamu tangu karne ya 7
- Huko Manchester ilianzishwa International Football Association Board, iliyoratibu sheria za kandanda (1882)
- Mfereji wa Suez ulitenganisha Afrika na Asia
- Uhamiaji wa umati wa watu katika nchi nyingine
- Mwanzo wa ujamaa na ukomunisti
- Papa Pius IX na Mtaguso wa kwanza wa Vatikano
- Ludwig van Beethoven, Frédéric Chopin, Richard Wagner na Franz Liszt, wanamuziki
- Louis Pasteur, mwanasayansi
- Guglielmo Marconi, aliyebuni redio
- Malkia Viktoria wa Uingereza
- Otto von Bismarck, Kansela wa Ujerumani
- Ndugu Lumière, waliobuni sinema
- Abraham Lincoln, rais wa Marekani aliyefuta utumwa nchini
- Charles Darwin (1809 - 1882), Mwingereza mwanasayansi
- George Stephenson aliyebuni treni
- Thomas Alva Edison aliyebuni taa na santuri
- Inabuniwa mota ya umeme
- Edward Jenner aliyebuni chanjo
- Inaanza kutengenezwa Coca-Cola
- Inaanza kutengenezwa aspirini
- Antonio Meucci aliyebuni simu
- Inabuniwa pikipiki
- Linabuniwa gari