Mata ogania
Mata ogania (pia maada ogania) ni mata inayotokana na viumbehai.
Asili ya mata ogania
[hariri | hariri chanzo]Viumbehai kama bakteria, mimea na wanyama huwa na miili inayofanywa na molekuli kubwa. Molekuli za viumbehai ni kubwa kwa sababu mchakato wa uhai unahitaji tabia kama uwezo wa kuzaa, kukua na umetaboli na shughuli hizo zinatekelezwa na molekuli za pekee mwilini zenye tabia maalumu.
Baada ya kifo cha kiumbehai, mchakato wa uhai ndani ya mwili wake unakwisha na molekuli za mwili zinaanza kuoza. Kuoza kunasababishwa mara nyingi na vyembehai au bakteria ndogo zinazoanza kula sehemu za miili ambayo imekufa na kupotewa na uwezo wa kujikinga dhidi ya bakteria hizo zinazopatikana muda wote lakini huzuiliwa na kinga za mwili hai.
Mchakato wa kuoza unavunja molekuli na kuacha kampaundi mbalimbali zisizotokea katika dunia peke yao isipokuwa kwa njia ya viumbehai. Kampaundi hizo zinaitwa kampaundi ogania na zina tabia ya kujengwa kwa atomi za kaboni zilizoingia katika muungo kemia na hidrojeni. Mchakato huu wa kuoza unaendelea kwa muda mrefu; kemikali kadhaa zinaachana haraka na mabaki ya mata ogania lakini kampaundi nyingine zinaweza kukaa kwa miaka elfu na zaidi ilhali zinaendelea kubadilika polepole.
Umuhimu wa kimsingi wa mata ogania
[hariri | hariri chanzo]Kuwepo kwa mada ogania duniani ni muhimu kwa viumbehai vilivyopo kwa sababu vinatunza nishati ndani yao na hivyo kuwa lishe kwao.
Kwa upande mwingine mata ogania huwa na tabia za kifizikia zinazotunza unyevu na maji kwenye udongo. Kwa njia hiyo kuwepo kwa mata ogania ni msingi wa uhai kwenye uso wa dunia.
Mata ogania katika udongo
[hariri | hariri chanzo]Mata ogania katika udongo (kwa Kiingereza: Soil organic matter / SOM) ni jumla ya mata ogania inayopatikana hasa kwenye tabaka la juu la udongo.
Kwa mfano wa msitu majani na matawi huanguka chini na kutandika ardhi ya msitu. Mabaki hayo yote ni mata ogania itakayoendelea kuoza na kubadilika. [1] Mara yameoza kiasi cha kwamba haionekani tena ilikuwa nini kiasili vipande vyake vinaingia ndani ya udongo wa juu ama kama wadudu na minyoo wanaoyasaga na kupeleka vipande kwenye makazi yao ndani ya udongo au kwa njia ya maji ya mvua yanayovibeba ndani ya nafasi katika udongo wa juu. Sasa imekuwa "mata ogania katika udongo". Mara hii mata imeendelea kuoza hadi kufikia hali ya kampaundi ogania za kudumu huitwa mboji (humus). [2]
Wanasayansi hutofautisha aina tatu za mata ogania katika udongo:
- biomasi ya viumbehai kama bakteria
- mabaki ya mimea (pia wanyama) yaliyopatikana kwa muda mfupi tu ambayo bado yako katika mchakato wa kuoza
- mboji ambayo ni mata ogania iliyooza tayari na kufikia hali ya kuwepo kwa kampaundi zisizoendelea kuchakata haraka.
"Mata ogania katika udongo huwa asilimia 1-6 ya masi ya udongo wa juu kwa sehemu kubwa ya ardhi ya sehemu za mwinuko.
Udongo wa juu wenye kiwango cha mata ogania chini ya asilimia 1 unapatikana hasa jangwani.
Kwa upande mwingine udongo wa juu kwenye tambarare za chini zenye maji mengi unaweza kushika hadi asilimia 90 za mata ogania. Udongo wenye asilimia 12-18 za kaboni ogania (sawa na asilimia 20-30 za mata ogania) huitwa udongo ogania" [3]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ http://www.epa.gov/epaoswer/non-hw/organics/index.htm
- ↑ Kwa hiyo kitaalamu "mata ogania katika udongo" ni mata ogania yote iliyopo ndani ya udongo isipokuwa mata ogania isiyoanza kuoza bado.(http://soils.usda.gov/sqi/concepts/glossary.html Archived 8 Novemba 2006 at the Wayback Machine.).
- ↑ Troeh, Frederick R., and Louis M. (Louis Milton) Thompson. Soils and Soil Fertility. 6th ed. Ames, Iowa: Blackwell Pub., 2005. [1] Archived 26 Oktoba 2014 at the Wayback Machine.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Aiken, George. United States of America. United States Geological Survey. Organic Matter in Ground Water. 2002. 1 May 2007 <http://water.usgs.gov/ogw/pubs/ofr0289/ga_organic.htm>.
- Cabaniss, Steve, Greg Madey, Patricia Maurice, Yingping Zhou, Laura Leff, Ola Olapade, Bob Wetzel, Jerry Leenheer, and Bob Wershaw, comps. Stochastic Synthesis of Natural Organic Matter. UNM, ND, KSU, UNC, USGS. 22 Apr. 2007.
- Cho, Min, Hyenmi Chung, and Jeyong Yoon. "Disinfection of Water Containing Natural Organic Matter by Using Ozone-Initiated Radical Reactions." Abstract. Applied and Environmental Microbiology Vol. 69 No.4 (2003): 2284-2291.
- Fortner, John D., Joseph B. Hughes, Jae-Hong Kim, and Hoon Hyung. "Natural Organic Matter Stabilizes Carbon Nanotubes in the Aqueous Phase." Abstract. Environmental Science & Technology Vol. 41 No. 1 (2007): 179-184.
- "Researchers Study Role of Natural Organic Matter in Environment." Science Daily 20 Dec. 2006. 22 Apr. 2007 <http://www.sciencedaily.com/releases/2006/12/061211221222.htm>.
- Senesi, Nicola, Baoshan Xing, and P.m. Huang. Biophysico-Chemical Processes Involving Natural Nonliving Organic Matter in Environmental Systems. New York: IUPAC, 2006.
- "Table 1: Surface Area, Volume, and Average Depth of Oceans and Seas." Encyclopædia Britannica.
- "Topic Snapshot: Natural Organic Material." American Water Works Association Research Foundation. 2007. 22 Apr. 2007 <http://www.awwarf.org/research/TopicsAndProjects/topicSnapShot.aspx?Topic=Organic Archived 28 Septemba 2007 at the Wayback Machine.>.
- United States of America. United States Geological Survey. Earth's Water Distribution. 10 May 2007. <http://ga.water.usgs.gov/edu/waterdistribution.html Archived 29 Juni 2012 at the Wayback Machine.>
- Water Sheds: Organic Matter. North Carolina State University. 1 May 2007 <http://www.water.ncsu.edu/watershedss/info/norganics.html Archived 14 Machi 2014 at the Wayback Machine.>.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mata ogania kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |