Tripoli
Mandhari
Tripoli ni neno la asili ya Kigiriki (Τρίπολις - Trípolis au Τρίπολη - Trípoli) linalomaanisha "miji mitatu" au "mji mwenye sehemu tatu". Asili yake ni maungano ya miji mitatu ya jirani kuwa mji au dola moja. Katika lugha ya Kiarabu neno limekuwa "Trablus" au "Tarablus" (طرابلس).
Neno linataja miji mbalimbali ya kisasa au ya kihistoria ndiyo hasa
- mji mkuu wa Libya, Tripoli (Libya) au Trablus/Libya
- mji wa pili wa Lebanon Tripoli (Lebanon) au Trablus/Lebanon
- mji wa Ugiriki, Tripoli (Ugiriki)
- mji wa Marekani, jimbo la Iowa, Tripoli (Iowa)
- mji wa Marekani, jimbo la Pennsylvania, Tripoli (Pennsylvania)
- jina la kihistoria la mji wa Tirebolu, Uturuki
- jina la kihistoria kwa dola ndogo katika Syria/Lebanon wakati wa vita za msalaba
- meli ya kijeshi ya Marekani USS Tripoli