Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Msaada wa kuanzisha makala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu kuchangia kwenye Wikipedia ya Kiswahili! Tayari ni Wikipedia kubwa ya Kiafrika - pamoja na lugha ya Afrikaans.
Pamoja na maelezo kwenye ukurasa huu unaweza kuangalia Mwongozo wa kuandika makala !

Kujiandikisha

Unaombwa kujiandikisha kwanza ingawa si lazima, lakini inasaidia! Maelezo yake ni hapa: Wikipedia:Mwongozo (Kujisajili).

Kutafakari na kupanga makala

Kabla ya kuanza panga makala yako. Wikipedia ni kamusi elezo.

  • Makala iwe ya maana. Usiaanzishe makala fupi mno yenye jina la mtu au mji tu halafu picha. Uwezekano ni mkubwa itafutwa. Hata makala fupi sana iwe angalau na sentensi moja kamili yenye habari kadhaa pamoja na alama ya {{Mbegu}}.
  • Si mahali pa kumsifu au kumpinga mtu au kitu chochote. Si mahala pa kusambaza maoni kama ukweli.
  • Tusiandike: Bwana fulani ni mwanamichezo bora wa Afrika. Hii ni hoja, si bayana ya hakika. Kama ni kweli na muhimu, andika ya kwamba kuna watu wanaomwona kama mwanamichezo bora. Lakini kama huwezi kutaja kwanza kwa nini amesifiwa hivyo uwezekano ni mkubwa ya kwamba sentensi kama hii itafutwa.
  • Tukumbuke ya kwamba tunaandika kwa ajili ya watu wote, si wataalamu pekee au vijana tu n.k. Makala ieleweke.
  • Tujaribu kuchukua msimamo wa kati yaani tueleze mitazamo na maoni mbalimbali yaliyopo kama ni muhimu.
Kibonye cha kutia sahihi
  • Tueleze chanzo cha habari zetu ikiwezekana.
  • Tusisahau kutia sahihi tukiandika kwenye ukurasa wa majadiliano wa makala au ukurasa wamtumiaji. Kuna kibonye chake kwenye dirisha la kuhariri. Heri tujiandikishe kwanza kwa jina la mtumiaji.

Kuhariri

Kuna njia mbili za kuhariri makala kwenye wikipedia.

  1. ukiwa na intaneti ya haraka bofya "Hariri" utaingia katika "Visual editor" inayofanana katika mengi na programu kama "Word"
  2. ukiwa na intaneti yenye kasi ndogo bofya "Hariri chanzo" unaingia katika hali ya kawaida.

Maelezo yanayofuata yanahusu njia ya kawaida.

Ukitaka kubadili, kusahihisha au kuhariri makala, ubonyeze "hariri chanzo" kule juu katika ukurasa wowote.

  • Ukitaka kubadilisha habari muhimu au mwelekeo wa makala ni vema kueleza nia yako kwanza katika ukurasa wa "majadiliano" wa makala ile. Umpe mwandishi wa awali nafasi ya kukujibu.
  • Ukisahihisha kosa ni vema kueleza sahihisho lako kifupi ama kwenye mstari wa "Muhtasari" (chini ya ukurasa wa "hariri") au kwenye majadiliano ya makala.
Alama hii (ndani ya duara nyekundu) kwenye dirisha la kuhariri linafanya kiungo kwa makala nyingine ya wikipedia

Viungo

Usiandike makala bila viungo, kwa sababu bila hivi maandishi yako hayatapatikana kwa mtu yeyote yatabaki siri yako tu!

Njia rahisi ya kuanzisha ni kutumia viungo vilivyopo bila makala. Haya yanaonekana kwa rangi nyekundu. Ukiona neno lenye rangi nyekundu maana yake ni ya kwamba mwandishi aliona inafaa kueleza jambo lile lakini hakuna makala bado. Ukibonyeza hapo utafungua ukurasa mpya na unaweza kuanza kuandika!

Kuanzisha makala mapya

Ukitaka kuanzisha makala mpya kabisa, andika jina katika dirisha la "tafuta" upande wa kushoto kando la dirisha. Gonga "Nenda" na wikipedia inatafuta makala kama ipo tayari kwa jina hili au la karibu. Kama haipo inaweza kuonyesha orodha ya makala mbalimbali ambako jina hili latokea - au hutaona orodha kama jina bado ni geni kabisa.

Lakini kwa namna yeyote utaona mstari "Create the page "(JINA)" on this wiki!" (JINA) ina rangi nyekundu. Bonyeza hapa na ukurasa mpya wa kuanzisha makala unajitokeza!

Kwa mfano, ukitaka kuanzisha ukurasa kuhusu "Plovdiv",

  • andika Plovdiv katika dirisha la "tafuta" na
  • kama makala haipo utaona mstari
  • "Anzisha ukurasa wa ""Plovdiv"" katika wiki hii! "
  • bonyeza neno nyekundu halafu ukurasa mpya wa kuhariri unafunguliwa na unaanza kazi!

Ukitaka kujua ufanye nini ili kusaidia kuboresha kamusi elezo hii, angalia Wikipedia:Makala za msingi za kamusi elezo utaona majina kwa rangi nyekundu haya ni makala yanyokosekana bonyeza tu na kuanza! Unasaidia pia ukiandika makala juu ya vichwa vya viungo vyekundu vinavyopatikana katika makala mengi kidogo.

Mpangilio wa makala

Ibara ya kwanza

Makala iwe fupi au ndefu lakini sentensi za kwanza ni muhimu hasa.

  • Zinaanza kwa Jina la makala linaloandikwa kwa herufi nene (teua jina halafu bonyeza B hapo juu kwenye dirisha la uhariri au taipu ''' kabla na mbele ya jina)
  • Sentensi za kwanza zionyeshe habari za kimsingi juu ya kichwa na mengine yafuata baadaye. Mfano: Usianze kwa "Chuo Kikuu cha XYZ kina wanafunzi 3500 kuna masomo ya ..." - afadhali: "Chuo Kikuu cha XYZ ni chuo cha kwanza (kipya, kikubwa n.k.) nchini ABC kilianzishwa mwaka 1234..."

Vichwa vya ndani ya makala

Makala ndefu bila mpangilio haivuti. Inasaidia sana ukiingiza vichwa. Hii ni rahisi! Utumie alama za = mbele na nyuma ya mstari wa kichwa.

==Kichwa kikubwa==
===Kichwa kidogo===

Picha

Ukitaka kutumia picha iliyopo katika Wikipedia ya lugha nyingine kuna njia mbili:

1. Picha iko tayari katika wikipedia commons au katika sw.wikipedia

Hii ni jambo la kujaribu! Fungua makala katika lugha nyingine yenye picha inayotakiwa, bonyeza "edit", nakili yote pamoja na mabano.

Kwa mfano: [[Image:Europe CD 3 036.jpg|right|300px|thumb|View over Paris from the Eiffel Tower]])

Hapo unahitaji kubadilisha Maelezo ambayo ni maneno ya mwisho kati ya | na ]]. Andika elezo kwa Kiswahili kwa mfano "Paris inayvoonekana kutoka mnara wa Eifel". Ukitaka kubadilisha ukubwa unabadilisha namba mbele ya "px". 200 px itakuwa ndogo zaidi, 100 px ndogo sana, 400 px kubwa zaidi - wakati mwingine tayari kubwa mno. Jaribu kwa kubonyeza hapo chini kabisa "Mandhari ya mabadilisho". Ukiona picha - sawa. Usipoona picha: haipo mahali inapopatikana. Jaribu nyjia ya pili!

2. Picha inachukuliwa kupitia kompyuta yako

a) hifadhi picha kwenye kompyuta unayotumia (kwa muda tu - baada ya kupakia unaweza kuifuta mara moja).

b) Jiandikishe kwa jina lako katika wikipedia ya Kiswahili. (bofya juu kulia, andika jina unalotumia)

c) chini kushoto utapata kiungo kinachoitwa "Pakia faili" (chini ya andiko "vifaa"). Bofya kiungo hicho.

d) Katika ukarasa ujao, unabofya kando la dirisha ndogo "Search" na kuteua faili ya picha kwenye kompyuta yako. Kwenye "summary" pakia anwani ya picha kwa mfano "http://en.wikipedia.org/wiki/Image:Europe_CD_3_036.jpg" kwa picha ya Paris. Halafu bofya "Upload file", na picha itakuwemo Wikipedia ya Kiswahili.

Unaweza kutumia picha kwa kuandika [[Image:jina_la_picha.jpg]].

Kuelekeza

Mara nyingi inatokea kwamba majina mawili yanafaa kwa makala fulani. Ikiwa hivi, lazima tuamue makala ipatikane chini ya jina gani. Lakini tunaweza kuelekeza kutoka jina jingine kwa jina sahihi la makala, ili watu waipate makala rahisi zaidi.

Ili kuelekeza kutoka jina moja kwenda jina sahihi la makala, tumia

#REDIRECT[[Jina la makala]]

Unaweza kuangalia mfano huu: Abunuwasi.

Jamii au Category

Usisahau kuunganisha makala yako na jamii au category. Jamii ni kama orodha ya makala zote chini ya kichwa fulani.

Kwa mfano makala zote kuhusu nchi za Afrika zimeorodheshwa katika jamii "Jamii:Nchi za Afrika". Tafuta jamii inayoweza kufaa (tazama ukurasa wa Mwanzo). Wengine watasaidia kupanga makala yako ikionekana jamii nyingine inafaa zaidi. Kwa maelezo zaidi angalia Msaada:Jamii.