Nenda kwa yaliyomo

Rozari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rozari pamoja na Biblia na Msulubiwa.

Rozari (kutoka Kilatini rosarium, yaani "taji la mawaridi"),[1] ni ushanga uliotengenezwa kwanza na Wakatoliki wa Karne za Kati ili kusali kwa kukariri Salamu Maria kadhaa pamoja na kutafakari mafumbo ya imani.

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Mafumbo 15 ya msingi ya Rozari na Bikira Maria wa Rozari.

Shanga zilitumika kama pambo tangu kale: barani Afrika zimepatikana za miaka 10,000 KK.

Lini na wapi zilianza kutumika kwa ajili ya sala haijulikani, lakini kuna sanamu ya karne ya 3 KK inayomuonyesha Mhindu akiwa na ushanga wa sala.

Lengo ni kutunza hesabu ya kauli ambazo zinakaririwa kwa kupitisha vidole viwili juu ya punje zilizounganishwa katika kamba au uzi.

Wakristo wa karne ya 15 waliotamani kusali kama watawa Zaburi 150, lakini hawakujua Kilatini au kusoma kabisa, walijifunza kwa urahisi kukariri Salamu Maria 150 huku wakitafakari mafumbo ya maisha ya Yesu, kama alivyowahi kufanya Dominiko wa Prussia (1382-1460), mmonaki Mkartusi.[2]

Lakini shirika lililojihusisha zaidi na Rozari ni lile la Wadominiko.[3][3][4][5][6]

Mwaka 1569, Papa Pius V aliyekuwa wa shirika hilo, alipitisha sala hiyo kwa Kanisa lote, akapanga mgawanyo wa mafumbo 15 na kukabidhi uenezi wake kwa Wadominiko wenzake.

Mafumbo hayo yaligawiwa katika makundi matatu: 5 ya furaha (utoto wa Yesu), 5 ya uchungu (mateso ya Yesu) na 5 ya utukufu (ufufuko wa Yesu na yatokanayo). Kila fumbo lina Salamu Maria 10, zikitanguliwa na Baba Yetu na kumalizika kwa Atukuzwe.

Mwaka 2002 Papa Yohane Paulo II alipendekeza kuongeza mafumbo 5 ya mwanga ili kuziba pengo kuhusu miaka ya utume wa Yesu.[7]

Mbali na hao, Mapapa wote walihimiza sala hiyo kama njia rahisi kwa wote ya kukumbuka na kuheshimu kazi ya wokovu iliyofanywa na Yesu Kristo.[8]

Sala hiyo imeenea katika baadhi ya madhehebu mengine ya Ukristo, hasa Anglikana.

Mafumbo ya Rozari

[hariri | hariri chanzo]
Mafumbo ya furaha
  1. Bikira Maria Kupashwa habari. Tunda: Unyenyekevu
  2. Bikira Maria kumtembelea Elizabeti. Tunda: Upendo kwa jirani
  3. Yesu kuzaliwa. Tunda: Ufukara
  4. Yesu kutolewa hekaluni. Tunda: Utiifu
  5. Yesu kupatikana siku ya tatu hekaluni. Tunda: Hekima
Mafumbo ya mwanga
  1. Ubatizo wa Yesu. Tunda: Uwazi kwa Roho Mtakatifu
  2. Arusi ya Kana. Tunda: Kwa Yesu kumpitia Maria
  3. Yesu akitangaza Ufalme wa Mungu. Tunda: Kumtegemea Mungu
  4. Yesu kugeuka sura. Tunda: Hamu ya utakatifu
  5. Yesu kuweka Ekaristi. Tunda: Ibada
Mafumbo ya uchungu
  1. Kihoro cha Yesu bustanini. Tunda: Chuki kwa dhambi
  2. Yesu kupigwa mijeledi. Tunda: Kiasi
  3. Yesu kutiwa taji la miba. Tunda: Ushujaa
  4. Yesu kubeba msalaba. Tunda: Uvumilivu
  5. Yesu msalabani. Tunda: Wokovu, Msamaha
Mafumbo ya utukufu
  1. Ufufuko wa Yesu. Tunda: Imani
  2. Yesu Kupaa mbinguni. Tunda: Tumaini
  3. Pentekoste. Tunda: Upendo kwa Mungu, utume
  4. Maria Kupalizwa mbinguni. Tunda: Neema ya kufa vema
  5. Maria kutukuzwa mbinguni. Tunda: Udumifu
  1. "Rosary". Wedgewood, Hensleigh. A Dictionary of English Etymology. 2nd ed. London: Trubner & Co., 1872. pg 544.
  2. McNicholas, J.T. "Alanus de Rupe". The Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company, 1907.
  3. 3.0 3.1 Thurston, Herbert, and Andrew Shipman. "The Rosary." The Catholic Encyclopedia. Vol. 13. New York: Robert Appleton Company, 1912. 7 Oct. 2014
  4. "Foley, Leonard O.F.M., "Our Lady of the Rosary", Saint of the Day, Lives, Lessons, and Feast, (revised by Pat McCloskey O.F.M.), Franciscan Media". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-11-08. Iliwekwa mnamo 2015-11-07.
  5. Cross, Frank Leslie; Livingstone, Elizabeth A. (2005). The Oxford Dictionary of the Christian Church. Oxford University Press. uk. 1427. ISBN 9780192802903. Iliwekwa mnamo 29 Aprili 2014. The rosary was propagated by the establishment of rosary confraternities, which were increasingly under Dominican control; in 1569, Pius V gave the Dominican Master General exclusive control over them. As a consequence, until 1984 the blessing of rosaries came to be reserved to Dominicans or priests having special faculties. Besides the Dominican rosary, there are various other forms. The Servite rosary, for instance, has seven sections in memory of the Seven Sorrows of the BVM, each consisting of the Lord's Prayer and seven Hail Marys; it apparently dates from the 17th cent. and was approved by the General Chapter of Servites in 1646.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Casanowicz, Immanuel Moses (1919). Ecclesiastical Art in the United States National Museum. U.S. Government Printing Office. uk. 632. Iliwekwa mnamo 29 Aprili 2014. Rosary.-Made of glass and composition beads. The full or greater Dominican rosary of 15 decades.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Apostolic Letter Rosarium Virginis Mariae". Iliwekwa mnamo 2007-02-10.
  8. Directory on Popular Piety and the Liturgy, 197 The Rosary, or Psalter of the Blessed Virgin Mary, is one of the most excellent prayers to the Mother of God
    • Popular Piety Besides sacramental liturgy and sacramentals, catechesis must take into account the forms of piety and popular devotions among the faithful. The religious sense of the Christian people has always found expression in various forms of piety surrounding the Church's sacramental life, such as the veneration of relics, visits to sanctuaries, pilgrimages, processions, the stations of the cross, religious dances, the rosary, medals, etc.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rozari kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.